Kocha JKT RUVU awapo moyo Wachezaji wake
Kocha mkuu wa timu ya JKT Ruvu, Fred Felix Minziro amewataka wachezaji wake kuonyesha uwezo wao mbele ya wageni waliosajiliwa na klabu zinazoshiriki ligi kuu ya Bara.Aidha Minziro amesema kuongezwa kwa idadi ya wachezaji wa kigeni katika usajili kutoka watano mpaka saba ni changamoto kwa Ruvu kuongeza bidii ili kufikia lengo la kumaliza katika moja ya nafasi tano za kwanza. Akizungumza na NIPASHE jana, Minziro alisema pamoja na idadi ya wageni katika timu za Bara kuongeza, ametaka wachezaji wake kutohofia hali hiyo bali kuona ni fursa ya kucheza kwa "jihadi ili waweze kupata namba katika kikosi cha timu ya taifa.
"Nimekuwa nikiwatoa wasi wasi wachezaji wangu wakati wa mazoezi ya kuwa wasihofie wachezaji wa kigeni." Alisema ili kuhakikisha kikosi chake kinafanya vizuri katika ligi kuu, amehamishia kambi mkoani Morogoro ili kutoa nafasi kwa wachezaji kufanya mazoezi ya kutosha kabla ya kuanza kwa ligi kuu Septemba 12.
Minziro alisema ingawa ligi itakuwa na ushindani mkubwa msimu ujao, amejipanga kumaliza katika nafasi nzuri ambayo itawawezesha kupata zawadi kutoka kwa wadhamini wakuu, kampuni ya Vodacom.
CHANZO: NIPASHE
Tweet
0 comments:
Post a Comment