Yanga kuendelea kumlisha Zutah
Uongozi wa Yanga umesema utaendelea kumhudumia kwa malazi, chakula na matibabu beki Mghana Joseph Zutah aliyeachwa muda mfupi baada ya kufuzu majaribio katika timu hiyo.Katibu Mkuu wa Yanga Dk. Jonas Tiboroha.
Zutah alisajiliwa na Yanga kwa mkataba wa miaka miwili akitokea Ghana, lakini ameshindwa kuendelea baada ya kiwango chake kutokubalika mashabiki na viongozi wa timu hiyo.
Akizungumza na NIPASHE jana, Katibu mkuu wa Yanga Jonas Tiboroha alisema ingawa wamevunja mkataba wa Zutah, Yanga itaendelea kumgharamia mahitaji muhimu ya kibinadamu wakati akisubiri kuondoka.
"Timu itaendelea kumsaidia huku tukiendelea kufanya mawasiliano na timu za Zimbabwe ambazo zimeonyesha nia ya kumsajili," alisema Tiboroha.
Alisema beki huyo anatarajiwa kuondoka nchini mara baada ya mchezo wao wa Ngao ya Hisani dhidi ya timu ya Azam, kwenye Uwanja wa Taifa Jumamosi ijayo.
Tiboroha alisema licha ya kuvunja mkataba, uongozi unaendelea kutoa ushirikiano kwa mchezaji huyo ili kuhakikisha anapata timu ya kwenda kucheza kabla ya kufungwa kwa dirisha la usajili Septemba 1.
"Hakuna anachotudai Zutah, tumemlipa kile alichotakiwa kulipwa ndani ya makubaliano ya mkataba."
CHANZO: NIPASHE
Tweet
0 comments:
Post a Comment