Simba yanasa Golikipa Mpya
Mabingwa wa zamani wa ligi kuu ya Bara, Simba wameingia mkataba wa miaka miwili na mlinda mlango wa Ivory Coast, Vincent Angban.Kocha Mkuu wa Simba, Dylan Kerr.
Kusajiliwa kwa kipa huyo mrefu kunaashiria kumalizika kwa uwepo wa misimu miwili wa Ivo Mapunda katika lango la Simba ambayo haijatwaa ubingwa wa Bara kwa miaka mitatu mfululizo.
Akizungumzana na NIPASHE jana, ofisa habari wa Simba Haji Manara alisema klabu imemsajili mchezaji huyo baada ya kumvutia kocha mkuu, Dylan Kerr ambaye aliutaka uongozi kumchukua baada ya majaribio mafupi.
Moja ya maombi ya Muingereza Kerr punde baada ya kuwasili nchini mwezi uliopita ilikuwa ni kupatiwa kpa mwingine baada ya kutoridhika na viwango vya Mapunda, Manyika Peter na yosso wa kikosi cha under 20, Dennis Richard.
Angban amesajiliwa baada ya kuonyesha kiwango kizuri katika mechi ya 'Simba Day' dhidi ya SC Villa ya Uganda Jumamosi iliyopita, alisema Manara.
Tangu Muivorycoast huyo adake mechi hiyo, hatma ya Mapunda ndani ya Simba imekumbwa na kiza kinene baada ya mchezaji huyo kudai kuwa uongozi umemnyima mkataba mpya licha ya kumlipa fedha za usajili, huku Simba ikidai kipa huyo wa zamani wa Yanga amewatosa.
“Kutokana na kiwango alichoonyesha Angban (siku ya Simba Day) hakuna timu ambayo ingekubali kumuacha," alisema Manara.
Baada ya kumpata kipa huyo, "sasa Simba yetu imetimia kila idara tunachosubiri ni ushindi katika ligi kwa kila timu tutakayokutana nayo.”
Kwa kumchukua Angban, Simba imefikisha wachezaji sita kati ya saba wa kigeni wanaoruhusiwa na kanuni. Wageni wengine ni Juuko Murshid (Uganda), Justice Majabvi(Zimbabwe), Simon Sserenkuma(Uganda), Hamis Kiiza(Uganda) na Emilly Nimuboma(Burundi).
CHANZO: NIPASHE
Tweet
0 comments:
Post a Comment