Sunday, 2 August 2015

Matokeo ya PSG vs Olympique Lyonnais kwenye Super Cup 2015 ilikuwa hivi

Wiki moja kabla ya kuanza kwa Ligi Kuu mbalimbali barani Ulaya kila Nchi huwa na utaratibu wa kucheza mchezo wa Hisani, Ufaransa na Ujerumani huwa wanaita Super Cup lakini kwa Uingereza wanaita Community Shield ambapo hukutanisha bingwa wa Ligi Kuu na bingwa wa Kombe la FA.

Ufaransa August 1 umepigwa mchezo wa Fainali ya Super Cup kati ya klabu ya Paris Saint Germain (PSG) dhidi ya klabu ya Olympique Lyonnais, mchezo uliopigwa katika dimba la Stade Saputo na klabu ya PSG kuibuka mabingwa wa kombe hilo baada ya kuifunga Olympique goli 2-0 Serge Aurier dakika ya 11 akipachika goli la kwanza huku goli la pili likiwekwa wavuni na Edson Cavani dakika ya 17.

0 comments:

Post a Comment

Copyright © 2014 KaribuVijana