Ishu tena inayosumbua ni kuhusu Rappa Birdman na Lilwayne katika msuguano
Ni mwezi mmoja umepita toka Lil Wayne na Birdman waziandike headlines baada ya ugomvi wao kuwa mkubwa kufikia Birdman kulipiga risasi Tour bus la Lil Wayne ili kumuua.
Polisi wanasema Birdman na rappa Young Thug walipanga na kushirikiana kisiri kumua Lil Wayne, Birdman aliamua kumpigia simu Lil Wayne na kumwambia kuwa yeye hakuhusika kwa njia yoyote ile kwenye tukio hilo.
Tetesi nyingi zilizosambaa ni kwamba Birdman alipokea simu kutoka kwa Young Thug na Jimmy Winfrey baada ya tukio hilo kutokea April 26 Atlanta lakini ripoti zinasema kwamba mtu kutoka kwenye kundi la Lil Wayne alimpigia simu Birdman kumtaarifu kuhusu tukio hilo.
Kuwapata watu waliohusika moja kwa moja imekuwa ngumu kwasababu ripoti zinasema kwa simu zote zilizopigwa zilikuwa chini ya jina la Birdman na zinalipiwa na Cash Money Records. Birdman bado anasema hakuhusika na tukio hilo.
Chanzo Millard ayo
0 comments:
Post a Comment