FIFA na Uchaguzi mwaka 2016
Yahusu shirikisho la soka duniani kuandaa kongamano la dharura mwaka ujao februari 2016,hii ni kutokana na sababu mbalimbali zikiwemo tuhuma za rushwa zinazowakabili maafisa wakuu wa shirikisho hilo Hii ni licha ya rais aliyeko sasa Sepp Blatter kutangaza nia ya kuondoka mamlakani wiki moja tu baada ya kuchaguliwa upya kuwa rais wa shirikisho hilo tarehe 26 mwezi Mei.Rais wa shirikisho la soka barani Ulaya (Uefa) Michel Platini, anadaiwa kupata shinikizo kutoka kwa viongozi wengi wa bara hilo kuwasilisha ombi lake la kuwa rais wa FIFA.
Kufikia wakati wa uchaguzi huo mpya Blatter atakuwa tayari keshahudumu kwa miezi tisa tangu atoe tangazo la kujiuzulu kufuatia shtuma kali za ufisadi dhidi ya shirikisho na haswa maafisa wakuu wa FIFA.mapema hii leo mpinzani wake mkubwa katika uchaguzi uliopita wa mwezi mei amemtaka kujiuzulu mara moja kiti hicho cha urais wa shirikisho hilo na pia tume maalumu iundwe kwa ajili ya kusimamia uchaguzi huo wa FIFA ujao
Tweet
0 comments:
Post a Comment