Friday, 4 September 2015

DAnnyWelbeck aumia kuwa nje mpaka Disemba

Mshambuliaji wa klabu ya Arsenal Danny Welbeck atakuwa nje ya Uwanja mpaka mwezi Disemba baada ya kufanyiwa upasuaji kwenye Goti .
Arsenal imeeleza kuwa matibabu kwenye Goti hilo hayakwenda vizuri na Wiki iliyopita ikaamuliwa afanyiwe operesheni.
Welbeck, aliumia Goti lake mwezi Aprili huku akiwa kaifungi timu yake ya Arsenal mabao 8 katika Mechi zake 34 tangu ahamie hapo kutoka Man United.
Hili ni pigo kubwa kwa Arsenal ambayo haikusajili mshambuliaji . Dirisha la usajili la kiangazi lilifungwa jumanne iliyopita.
Mfaransa Oliver Giroud anabaki kuwa mshambuliaji pekee wa kutumainiwa katika kikosi hicho.







Djilobodji aachwa nje ya kikosi cha Chelsea

Mchezaji aliyesajiliwa hivi majuzi na Chelsea, Papy Djilobodji, ameachwa nje ya kikosi cha klabu hiyo kitakachocheza mechi ya ligi ya klabu bingwa Ulaya, hatua ya makundi.
Mlinzi huyo Djilobodji,mwenye umri wa miaka 26, kutoka Senegal, alisajiliwa na 'the Blues' siku ya mwisho ya kuhama wachezaji kutoka klabu ya Nantes ya Ufaransa kwa £4m.
Wachezaji wenzake waliojiunga majuzi na mabingwa hao wa Uingereza, Asmir Begovic, Abdul Rahman Baba, Pedro na Radamel Falcao wote wamejumuishwa kwenye kikosi hicho cha wachezaji 25.
Nyota huyo aliachwa nje kwa kuwa Chelsea, walikuwa tayari wamejaza nafasi za wachezaji ambao sio wazaliwa wa Uingereza kwenye kikosi chao cha kwanza.
Mlinda lango wa Manchester United David De Gea, yumo kwenye kikosi cha kilabu hiyo baada ya mpango wa kuhamia Real Madrid kutibuka.








Enyema ajiondoa kutoka kikosi cha Timu ya Taifa ya Nigeria

Mshambuliaji wa klabu ya Arsenal Danny Welbeck atakuwa nje ya Uwanja mpaka mwezi Disemba baada ya kufanyiwa upasuaji kwenye Goti .
Arsenal imeeleza kuwa matibabu kwenye Goti hilo hayakwenda vizuri na Wiki iliyopita ikaamuliwa afanyiwe operesheni.
Welbeck, aliumia Goti lake mwezi Aprili huku akiwa kaifungi timu yake ya Arsenal mabao 8 katika Mechi zake 34 tangu ahamie hapo kutoka Man United.
Hili ni pigo kubwa kwa Arsenal ambayo haikusajili mshambuliaji . Dirisha la usajili la kiangazi lilifungwa jumanne iliyopita.
Mfaransa Oliver Giroud anabaki kuwa mshambuliaji pekee wa kutumainiwa katika kikosi hicho.







Dimitar Berbatov katika klabu ya PAOK ya Ugiriki katika picha za mapokezi


Mshambuliaji huyo wa Kibulgaria mwenye umri wa miaka 34 amejiunga na klabu hiyo kwa mkataba wa miaka miwili akitokea katika klabu ya AS Monaco. Dimitar Berbatov ameingia katika usajili wa kihistoria wa klabu ya PAOK baada ya kusaini mkataba wa miaka 2.


Mara nyingi katika Ligi kubwa duniani mshambuliaji anayefanyiwa utambulisho maalum uwanjani ni yule mwenye jina kubwa pamoja na uwezo mkubwa uwanjani, licha ya Berbatov kuonekana kaisha uwanjani, kwa upande wa Ugiriki Septemba 3 ilikuwa ni siku yake maalum ya kutambulishwa mbele ya mashabiki 10000 katika uwanja wa Toumba.







Mourinho, Ronaldo na Smalling wameingia katika kitabu cha Guinness World Records



Baadhi ya wanamichezo duniani akiwemo Jose Mourinho, Frank Lampard na Cristiano Ronaldo wameingia katika kitabu cha kipya cha Guinness World Records ambacho toleo jipya litatoka Septemba 10, Mastaa hao wamepewa heshima ya kuwemo katika kitabu hicho kutokana na rekodi zao mbalimbali.

Jose Mourinho ndio ameingia katika headlines kubwa zaidi baada ya kupewa Tuzo za Guinness World Records mara nne, hivyo ana rekodi nne tofauti zitakazo mfanya aandikwe katika kitabu hicho.

Kocha huyo wa Chelsea ameweka rekodi ya kuwa kocha wa klabu ya kwanza kumaliza msimu akiwa na point 95, kocha aliyeshinda Kombe la Ligi ya Mabingwa mara nyingi akiwa na klabu mbili tofauti (2), ndiye kocha mwenye umri mdogo aliyewahi kucheza mechi 100 za Ligi ya Mabingwa ilikuwa kipindi ana miaka 49 na siku 12,

Mourinho pia ana rekodi ya kutofungwa katika uwanja wa nyumbani mara 77 hii ni katika mechi za Ligi Kuu. Hata hivyo Cristiano Ronaldo ameingia katika rekodi ya kuwa mchezaji aliyeshinda hat-tricks 27 katika mechi za Laliga.

Beki wa klabu ya Manchester United yumo pia kwa rekodi ya kuwa mchezaji aliyetokea benchi na kufunga goli la mapema dakika ya 5 na sekunde 9 baada ya kuingia, ilikuwa dhidi ya Burnley msimu uliyopita, Smalling alijiongezea rekodi kwa kufunga goli la pili hivyo anatajwa kama mchezaji aliyetokea benchi na kufunga magoli mengi.








Saturday, 29 August 2015

Hotuba ya Edward Lowassa katika Uzinduzi wa ilani ya Uchaguzi ya Ukawa 29 August 2015

Mgombea Urais wa Tanzania ndani ya Ukawa kupitia Tiketi ya CHADEMA Edward Lowassa




Copyright © 2014 KaribuVijana