Lowassa awatuhumu CCm wezi wa kura
Mgombea wa Urais kupitia CHADEMA Edward Lowassa ameituhumu CCM kuwa ni hodari wa kuiba kura, hivyo akawataka wananchi kujitokeza kupiga kura ili hata sehemu ya kura hizo ikiibiwa UKAWA ishinde kwa kishindo.Lowassa ambae ni Waziri Mkuu wa zamani aliwaambia umati wa wafuasi wa UKAWA waliojitokeza jana katika ofisi ya makao makuu ya CUF yalioko Buguruni kuwa ili kufanikisha ushindi hawana budi kushirikiana kushawishiana na kupiga kura kwa wingi na kuzilinda October 25,kauli hiyo ya Lowassa ambae amelelewa na CCM tangu alipojiunga akiwa mdogo mwaka 1977 ameendeleza tuhuma ambazo hutolewa na vyama vya upinzani kwamba chama hicho huchakachua matokeo wakati wa Uchaguzi.
Tweet
0 comments:
Post a Comment