Friday, 7 August 2015

Edin Dzeko Kuhamia AS Roma ya Italia

Mshambulaiji wa klabu ya Man City, Edin Dzeko amewasili mjini Roma nchini Italia, tayari kwa kufanyiwa vipimo vya afya kablA ya kukamilisha usajili wa kujiunga na klabu ya AS Roma mwishoni mwa juma hili.

Dzeko alipata mapokezi makubwa kutoka kwa mashabiki wa klabu hiyo inayotumia uwanja wa Olympico uliopo mjini Roma, na wanaamini ujio wa mshambuliaji huyo huenda ukawa mkombozi wa mafanikio wanayo yahitaji.

Uongozi wa klabu ya Man City tayari wameshakubaliana na As Roma ada ya usajili wa paund million 14, kwa mshambuliaji huyo kutoka nchini Bosnia na taratibu za malipo zitafanyika mara baada ya kukamilika kwa mipango ya vipimo vya afya.

Dzeko, ameelekea nchini Italia huku akiacha kumbu kumbu kwa mashabiki wa klabu ya Man City, baada ya kuwa kinara wa upachikaji wa mabao katika msimu wa 2012-13.

Katika msimu huo ambao ilikua ni mara ya kwanza kwa Dzeko kucheza ligi ya nchini England, akiwa na Man City baada ya kusajiliwa akitokea Wolfsburg nchini Ujerumani alifanikiwa kufunga mabao 15 na katika michuano yote aliyocheza alifunga mabao 26.

Kuondoka kwa Dzeko, kunaacha maswali mengi kwa mashabiki wa klabu ya Man City, kutokana na mchezo wa ufunguzi wa ligi utakaowakabili mwanzoni mwa juma lijalo dhidi ya West Brom, kwani mpaka sasa hakuna mshambuliaji wa kutumainiwa kikosini kufuatia Sergio Aguero kuwa majeruhi.

Meneja wa Man City mpaka sasa ameshindwa kufanya usajili wa mshambuliaji ambaye ataziba pengo la Dzeko, hali ambayo inaendelea kuzusha hofu kubwa kwa mashabiki.

Mshambuliaji Edin Dzeko






0 comments:

Post a Comment

Copyright © 2014 KaribuVijana