Angel Di Maria atua rasmi Ufaransa
Mabingwa wa Ufaransa Angel Di Maria hii leo wamethibitisha kukamilisha usajili wa winga raia wa Argentina Angel Di Maria .Klabu hiyo ya Ufaransa imekubali kulipa ada ya uhamisho ya paundi milioni 45 kwa klabu yake ya zamani Manchester United kiasi ambacho ni hasara ya paundi milioni 10.
United ilimnunua Di Maria kwa ada ya uhamisho ya paundi milioni 55 na kumfanya kuwa mchezaji ghali kuliko wote kwenye historia ya ligi ya England .
Di Maria anaondoka United akiwa amecheza kwa msimu mmoja pekee akiwa amesajiliwa toka klabu ya Real Madrid.
Winga huyu ametia saini mkataba wa miaka minne ambao utamuweka ndani ya klabu hii ya Ufaransa mpaka mwaka 2019 .
Tweet
0 comments:
Post a Comment