Wednesday, 22 July 2015

kiongozi kundi la kigaidi auwawa nchini syria

Mmoja wa wajumbe wa bunge la congress amesema kuawawa kwa mtu huyo Al Fahdli mwenye ufahamu na gaidi hatari ambaye amekuwa akijaribu kuiangamiza Marekani na washirika wake ni faraja kubwa.

Al Fahdli anajulikana kama mtu muhimu katika Khorasan ambao ni mtandao muhumu kwa kundi la kigaidi la Al Qaeda ambalo lilikuwa likitumwa kutokea Pakistani na Syria kwa ajili ya kufanya mashambulizi ya kigaidi kwa nchi za magharibi.

Mfadhili huyo mkubwa wa kundi la kigaidi amekuwa akitafutwa na marekani kwa mara kadhaa ambapo Marekani ilitangaza kitita cha dola milioni saba kwa yoyote atakayefanikishwa kuuawa kwake.

Msemaji wa Wizara ya Ulinzi ya Marekani Pentagon anasema Al Fahdli alikuwa miongoni mwa watu wachache wanaoaminiwa na kiongozi wa Al Qaeda ambaye pia aliwahi kupewa taarifa za kutokea kwa shambulio la kigaidi septemba 11 huko Marekani.

Taarifa za kifo chache zilisambazwa tangu mwaka jana lakini ni sasa imethibitishwa kuwa Al Fahdli ameuawa Julai 8 mwaka huu huko Syria.




chanzo BBC

0 comments:

Post a Comment

Copyright © 2014 KaribuVijana