Wednesday, 22 July 2015

Buhari tayari kwa Majadiliano na kundi la Boko Haram

Rais wa Nigeria Muhammadu Buhari amesema kuwa yuko tayari kufanya mazungumzo na wanamgambo wa kiislam wa Boko Haram ili wawaachilia wasichana wa wa shule 219 waliotekwa nyara kutoka kwenye shule yao ya malazi mnamo mwaka 2014.

"Kama tunaamini kuwa uongozi wa Boko Haram unaweza kuwaachilia huru na salama wasichana hao tunaweza kujiandaa kufanya kuzungumzia nini wanachokitaka ," alikua akizungumza katika mahojiano na televisheni ya Marekani CNN.


Kundi la wanamgambo wa kiislam la Boko Haram limekua likiendesha mashambulizi ya mara kwa mara katika maeneo ya kaskazini mwa Nigeria na serikali imekuwa ikilaumiwa kwa kutoweza kuwadhibiti wanamgambo hao wa kiislam wenye itikadi kali.

Rais wa Nigeria Muhammadu Buhari





Rais wa Nigeria Muhammadu Buhari akiwa na Rais wa Marekani Barack Obama wakati wa ziara yake nchini Marekani





Chanzo BBC



0 comments:

Post a Comment

Copyright © 2014 KaribuVijana